Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 8 Novemba 2015

AGANA NA UMASAKINI KUPITIA KILIMO CHA MATIKITI WENGI KIMEWASAIDIA

UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI- WATERMELON PRODUCTION

UTANGULIZI
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.  Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga  inayotambaa.  Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama  matango,maboga na maskwash.  Zao la tikiti maji  ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa  na kuhudumiwa  vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.
HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.  Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua:  kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu  mpaka wa tisa.
UANDAAJI WA SHAMBA
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.

UPANDAJI
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja  katika kila  shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi  na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)UPUNGUZAJI WA MIMEA
Mimea ya michikichi huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo  katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.
Aangalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.
Wakati  mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.MATANDAZO (MULCHES)
Matandazo ina maana ya kutumia  nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche  kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu  kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbolea za viwandani aina ya  NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana.  Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.
UMWAGILIAJI
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache.  Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie  juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.
MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume  huwa  ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.  
Hii hufanywa kwakukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.

Tikiti maji ni mboga/tunda linalolimwa hasa katika maeneo ya joto lenye kiwango cha joto cha 22-28 0c na mvua 600 - 400mm kwa mwaka. 

Mbali na kuwa na faida mbali mbali kiafya tikiti maji linaweza kumtoa mkulima wa kawaida katika umaskini. Hii kutokana na sababu zifuatazo.


1. Tikitimaji ni zao la bustani linalochukua miezi 3-4 kuvunwa, hvyo kwa mwaka linaweza kuvunwa mara 3 hadi 4.
2. kwa ekari moja mavuno ya tikiti maji ni matunda 2000 - 8000  au zaidi kwa miezi 3-4 kutokanana uangalizi wa mkulima katika shamba ikiwa ni kutumia mbolea kama inavyo takiwa, kuzuia wadudu na magonjwa, n.k. Pamoja na nafasi iliyotumika katika upandaji (1x1m, 2x2m, 1.5 x 1.5m).

JINSI YA KUJUA FAIDA
Katika maeneo mengi ya Tanzania bei ya tikiti maji lenye sifa nzuri ni 2,000/=  - 3,000/=

kwa bei ya 2,000/= na mavuno ya 2000 matunda/ekari (Matunda mazuri)
- Baada ya mavuno utajipatia kiwango cha chini kisichopungua jumla ya Tsh.4,000,000/= kwa mwaka ni 12,000,000/= kwa mavuno ya mara tatu kwa mwaka kwa ekari.

Gharama hii itaenda juu zaidi ama itapungua kutegemea na idadi ya matunda uliyoyapata katika ekari mmoja na bei ya muuzaji. Hivyo unaweza ukapata faida kubwa zaidi ukiongeza uangalizi wa shamba lako na kufuata utaratibu katika ulimaji wa zao hili.

  MAHITAJI
Tikiti maji linahitaji mbolea, maji, kemikali za kuua wadudu na magonjwa pamoja na maandalizi mabali mbali ya shamba ambavyo gharama yake haizidi Tsh. 500,000/= katika uangalizi mkubwa

FAIDA
Hivyo mkulima katika uangalizi wa mzuri ana uhakika wa kupata faida ya Tsh. 3,500,000/=  na zaidi kila baada ya miezi 3-4. 


Ushauri: Kwa mafanikio mazuri na kuinuana kiuchumi wakulima wakiungana na kufanya kilimo bishara watakuwa na nafasi kubwa ya mafanikio kwa maana kiuchumi wanataweza kusaidiana ili kuinua mtaji na kuweza kupata kiasi cha kuanzia shughuli zao za kilimo. 
Jikomboe katika umaskini na kilimo cha bustani:

Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuanza kilimo cha bustani wasiliana nasi kupitia, mickyando12@gmail.com ama 0675933114

Asante


9 comments:



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni