Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 3 Desemba 2015

WENGI WAMENUFAIKA KUPITIA KILIMO CHA UFUGAJI WA KUKU WAKIENYEJI SOMA APA ILI UKUZE KIPATO CHAKO ILI UKIENDELEA NA SHUGHULI NYINGINE

Downloadable Version:Ufugaji Wa Kuku Wa Kienyeji Kama Mradi
MAHITAJI
  1. Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01
  2. Banda bora
  3. Vyombo vya chakula na maji
  4. Chakula bora
  5. Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa
  6. Chanzo cha nishati joto na mwanga
  7. Elimu na ujuzi wa malezi bora
  8. Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
  9. Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa)
  10. Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu
KUKU 10
Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa. Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.
Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri mmoja pia.
JOGOO 01
Jogoo mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote kumi. Hakikisha katika uchaguzi wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu, uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vema mfugaji akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake. Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora wa jogoo aliyechaguliwa.
BANDA BORA
Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04. Yani urefu uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa unaolingana. Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira husika. Mfano katika maeneo ambayo fitoKuku zinapatikana kwa urahisi banda linaweza kuandaliwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo. Au sehemu ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi. Vifaa vya kujengea banda vizingatie pia gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
  • Sakafu: Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
  • Kuta: Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi,udongo, matofali, mawe, mabati na wavu
  • Paa: Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.
  • Wigo: Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi, matete, wavu na mabati
Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
  • Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari.
  • Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
  • Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
  • Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala.
  • Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.
  • Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.
  • Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa. Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.
JINSI YA KUFANYA
Wakuze kuku wako hadi watakapofikia muda wa kutaga. Wakianza kutetea ni kiashiria kwamba wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia.
Viota vinapaswa viwe na ukubwa stahiki ili kumwezesha kuku kuyafunika mayai yote vizuri wakati wa kuetamia, viota viwe vinavyozuia mayai kutawanyika, viwe mahali pakavu na safi.
Hakikisha kuku wote wanataga katika viota tofauti. Kuku anapotaga IMG_20140306_153739mayai matatu unapashwa kuchukua mayai mawili na kumwachia yai moja ili kumfanya aendelee kutaga zaidi. Kuku akifikia yai la kumi na mbili anza kumwachia mayai matatu ili kumwandaa kwa kazi ya kuetamia. Kwa kufanya hivi, kuku atataga mayai 15 au zaidi na ikiwa atataga mayai 15 au chini ya hapo nakushauri utafute mayai mengine ujazilizie ili kufikisha mayai 20 kwa kila kuku. Zingatia kwamba mayai unayoyatoa kwa kila kuku, yanatunzwa sehemu salama, mahali pakavu, pasafi na penye joto la wastani.
Kuku wote wanapaswa kuanza kuetamia kwa siku moja. Ili kufanikisha hili inapasa uwe karibu na kuku wako. Kuku mmoja akianza kuetamia mwekee mayai ya kuku wa kisasa au mayai mabovu ya kuku wa kienyeji. Utafanya hivi hadi kuku wako wote watakapoanza kuetamia mayai. Kuweka mayai mabovu au mayai ya kuku yaliyotumika humfanya kuku aendelee kuetamia akijua ni mayai yake.
Baada ya kuona kwamba kuku wako wote wapo tayari kwa kuetamia mayai, waandalie banda maalumu kwajili ya kuetamia yani chumba kimoja katika lile banda letu. Ninashauri kwamba chumba kwajili ya kuetamia kiwe chumba cha kwanza au cha mwisho katika mfuatano wa vyumba vya banda lako. Andaa viota bora vya kuetamia, weka mayai 20 kwa kila kiota, ikiwa hayajatimia unaweza kununua kwa wafugaji wengine ili kuifikia idadi yako.
Waamishe kuku kutoka wanapotagia na kuwaweka katika chumba ulichokiandaa kwajili ya kuetamia. Ili ufanikiwe katika zoezi hili inafaa lifanyike wakati wa usiku na unafanya katika giza. Mweke kuku katika kila kiota na asubuhi wajikute kila mmoja katika kiota chake. Wahudumie kwa chakula na maji ya kutosha. Wakati wa usiku waongezee joto la ziada kwa kuweka jiko au ndoo ya chuma yenye chengachenga za mkaa au kama una umeme weka taa za joto.
Baada ya siku 21-25 kuku wako wataanza kuangua vifaranga. Huu ndio wakati unaotakiwa kuwa karibu sana na kuku wako kuliko wakati wote. Watenge vifaranga mara tu baada ya kuanguliwa; waweke katika chumba chao maalumu mbali na kuku. Kama chumba cha kuetamia kilikuwa cha kwanza basi vifaranga wawe chumba cha mwisho n.k
Ukishawatenga vifaranga mbali na matetea wako, wawekee tena mayai mengine 20 kila tetea, mayai ambayo utayanunua kwa wafigaji wenzako. Hakikisha kuku waliotaga hayo mayai ni wazuri, hawana magonjwa na wanauzito/ukubwa unaofaa. Mayai yote yakaguliwe vizuri ili kujua kwamba yameharibika, yana nyufa au mabovu. Kabla ya kuweka mayai mengine hakikisha chumba chako ni kisafi na viota vimesafishwa, havina wadudu na uchafu wowote. Kuku wako bila kujijua wataanza kuetamia upya mayai uliowawekea.
Ukiwawekea mayai rudia mzunguko kama nilivyokwambia awali. Baada ya siku 21 hadi 25 tena utapata vifaranga wako wengine tena. Fuata kila hatua kama nilivyokwambia hapo awali. Lakini kwa awamu hii nashauri waache matetea wako wapumzike wala usiwapatie mayai mengine tena.
JINSI YA KULEA VIFARANGA
Ikikaribia siku ya 20 tangu ulipowawekea matetea wako mayai katika chumba cha kuetamia, andaa chumba kwa ajili ya kulea vifaranga. Safisha kwa kuondoa uchafu na wadudu wote.
Washa taa ya joto au weka chombo cha kutoa joto katika chumba cha vifaranga nusu saa kabla hujaIMG_20141114_104757anza kuingiza vifaranga wako. Weka pia chakula na maji ya kutosha katika vyombo vyenye umbile na ukubwa utakaowawezesha vifaranga kuvitumia. Tandaza magazeti, maboksi, makaratasi n.k katika sakafu ya chumba hicho. Hakikisha vifaranga wako hawajikusanyi sehemu moja maana wakifanya hivyo wengi wao watakufa ili ufanikiwe katika jambo hili, banda lako liwe la mduara katika kona zake.
Weka joto la kutosha. Joto la kutosha ni lile linalowafanya vifaranga watawanyike chini ya chanzo cha joto wakati kama joto limezidi vifaranya kukimbia mbali na chanzo cha joto na ikiwa joto halitoshi vifaranga hujukusanya chini ya chanzo cha joto.
Baada ya siku 3 utawapatia chanjo ya Gumboro na siku 7 wapatie chanjo ya New Castle, utarudia tena kuwapa chanjo hii baada ya mwezi mmoja kisha utafanya hivi kila baada ya miezi mitatu mitatu.
MAPATO YA MRADI WAKO
Katika uzazi wa kwanza utapata vifaranga 150 kwa wastani wa vifaranga 15 kwa kila kuku. Tuseme haujazingatia kanuni za ufugaji za makala hii ukapata vifaranga 100 yani wastani wa vifaranga 10 kwa kila kuku. Kisha baadaye wakakua wakafa kuku 50 yani watano kwa kila kuku utakuwa na jumla ya kuku 50.
Baada ya wiki 3 utapata tena kuku tufanye kwa mahesabu kama hayo hapo juu kwa hasara utakuwa na kuku wengine 50, na kufanya jumla ya kuku 100. Ikiwa kuku wako baada ya uzao wa pili uliwapumzisha kwa miezi miwili basi mwezi wa 3 utapata tena kuku vifaranga 100 na wiki 3 baadaye utapata wengine 100. Kwa mahesabu kama hayo awali wakikuwa utakuwa na kuku wengine 100 ambao watakuwa.
Baada ya miezi 6 utakuwa na kuku wakubwa wa uzao wa kwanza 50, uzao wa pili kuku 50 na utakuwa na kuku wenye umri wa miezi mitatu 50 wa uzao wa 3 na kuku wengine 50 wa uzao wa 4.
Katika kuku 100 wa uzao wa kwanza na pili, tufanye kuku 50 wawe matetea ukijumlisha na kuku 10 ulioanza nao mradi utakuwa na matetea 60. Ikiwa kila tetea atatotoa vifaranga 10 na vikakua vitano tu, mwishoni utakuwa na kuku 300 na baada ya miezi mitatu kuku wengine 900 toka katika kutoka kwa uzao wa kwanza, wapili na watatu. Hivyo mwaka wa pili utafunga na kuku si chini ya 1,200/= wanaotaga mayai.
Ukiuza majogoo yote 1,200/= kwa bei ya 8,000/= ili upate pesa ya kujenga miundombinu bora maana sasa utakuwa na kuku wengi wanaoendelea kuzaliana kwa kasi utapata pesa kiasi cha TZS 7,200,000/=. Sasa ongeza kuku wako wa kutaga hadi wafikie kuku 4,000 maana sasa utakuwa na pesa za kutosha kuendesha mradi wako.
IMG_20140309_101614Sasa ukiwa na kuku 4000 wa kienyeji wa kutaga mayai, ikiwa kuku 3000 tu watataga ukauza yai moja kwa bei ya haraka haraka ya TZS 250 tu, utapata TZS 750,000/= kwa siku ambayo sawa na TZS 22,500,000/= kwa mwezi na TZS 270,000,000/= kwa mwaka sawa sawa na 128,572 USD. Kumbuka mwamba makadilio haya niya chini sana. Ukifata kanuni zote kwa makini na maombi huku ukimtanguliza Mungu utafikia hata TZS 500,000,000/= kwa mwaka.
Kumbuka unapofanikiwa kupata mapato ya kila aina, umtolee Mungu zaka(x10%) ya mapato yako, pia ukatoe sadaka ambayo ni kubwa kuliko zaka na uwasaidie masikini na wahitaji.
Tunza kumbukumbu zako zote za fedha katika daftari maalumu kuhusu mapato na matumizi ya mradi wako. Pia hali ya kuku wako kuhusu tarehe za chanjo ya mwisho, siku walipoanza kuetamia, magonjwa yanayowasumbua mara kwa mara n.k
Wasiliana nasi kwa maswali, maoni au ushauri.

Jumanne, 17 Novemba 2015

<table border="0" cellpadding="1" cellspacing="0"><tr><td align="center"><a href="http://www.chathour.com" style="font-family: Arial, Helvetica; font-size: 12px;">Chat Hour</a> - <a href="http://www.chathour.com" style="font-family: Arial, Helvetica; font-size: 12px;">free chat

Jumapili, 8 Novemba 2015

AGANA NA UMASAKINI KUPITIA KILIMO CHA MATIKITI WENGI KIMEWASAIDIA

UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI- WATERMELON PRODUCTION

UTANGULIZI
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.  Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga  inayotambaa.  Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama  matango,maboga na maskwash.  Zao la tikiti maji  ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa  na kuhudumiwa  vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.
HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.  Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua:  kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu  mpaka wa tisa.
UANDAAJI WA SHAMBA
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.

UPANDAJI
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja  katika kila  shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi  na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)UPUNGUZAJI WA MIMEA
Mimea ya michikichi huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo  katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.
Aangalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.
Wakati  mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.MATANDAZO (MULCHES)
Matandazo ina maana ya kutumia  nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche  kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu  kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbolea za viwandani aina ya  NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana.  Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.
UMWAGILIAJI
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache.  Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie  juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.
MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume  huwa  ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.  
Hii hufanywa kwakukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.

Tikiti maji ni mboga/tunda linalolimwa hasa katika maeneo ya joto lenye kiwango cha joto cha 22-28 0c na mvua 600 - 400mm kwa mwaka. 

Mbali na kuwa na faida mbali mbali kiafya tikiti maji linaweza kumtoa mkulima wa kawaida katika umaskini. Hii kutokana na sababu zifuatazo.


1. Tikitimaji ni zao la bustani linalochukua miezi 3-4 kuvunwa, hvyo kwa mwaka linaweza kuvunwa mara 3 hadi 4.
2. kwa ekari moja mavuno ya tikiti maji ni matunda 2000 - 8000  au zaidi kwa miezi 3-4 kutokanana uangalizi wa mkulima katika shamba ikiwa ni kutumia mbolea kama inavyo takiwa, kuzuia wadudu na magonjwa, n.k. Pamoja na nafasi iliyotumika katika upandaji (1x1m, 2x2m, 1.5 x 1.5m).

JINSI YA KUJUA FAIDA
Katika maeneo mengi ya Tanzania bei ya tikiti maji lenye sifa nzuri ni 2,000/=  - 3,000/=

kwa bei ya 2,000/= na mavuno ya 2000 matunda/ekari (Matunda mazuri)
- Baada ya mavuno utajipatia kiwango cha chini kisichopungua jumla ya Tsh.4,000,000/= kwa mwaka ni 12,000,000/= kwa mavuno ya mara tatu kwa mwaka kwa ekari.

Gharama hii itaenda juu zaidi ama itapungua kutegemea na idadi ya matunda uliyoyapata katika ekari mmoja na bei ya muuzaji. Hivyo unaweza ukapata faida kubwa zaidi ukiongeza uangalizi wa shamba lako na kufuata utaratibu katika ulimaji wa zao hili.

  MAHITAJI
Tikiti maji linahitaji mbolea, maji, kemikali za kuua wadudu na magonjwa pamoja na maandalizi mabali mbali ya shamba ambavyo gharama yake haizidi Tsh. 500,000/= katika uangalizi mkubwa

FAIDA
Hivyo mkulima katika uangalizi wa mzuri ana uhakika wa kupata faida ya Tsh. 3,500,000/=  na zaidi kila baada ya miezi 3-4. 


Ushauri: Kwa mafanikio mazuri na kuinuana kiuchumi wakulima wakiungana na kufanya kilimo bishara watakuwa na nafasi kubwa ya mafanikio kwa maana kiuchumi wanataweza kusaidiana ili kuinua mtaji na kuweza kupata kiasi cha kuanzia shughuli zao za kilimo. 
Jikomboe katika umaskini na kilimo cha bustani:

Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuanza kilimo cha bustani wasiliana nasi kupitia, mickyando12@gmail.com ama 0675933114

Asante


9 comments:



Ijumaa, 6 Novemba 2015

KILIMO CHA VITUNGUU;FAIDA NA SOKO LA VITUNGUU

MAELEZO YA MSINGI KUHUSU KILIMO CHA VITUNGUU

Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake. Hulimwa nyanda za baridi kwa wingi sana. Nyanda zenye joto vitunguu hulimwa pia. Tanzania vitunguu hulimwa sana sehemu za Mang’ula, Mgeta na Singida. Hata hivyo vitunguu hustawi maeneo mengi ya Tanzania.
FAIDA YA VITUNGUU
Vitunguu vinamwezeshsa mkulima kukuza kupato kwa haraka kama atazingatia masharti yake,vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana. Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin C na vitamin E.

Halijoto
 Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo.

Udongo na mahitaji ya maji
Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga. Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji. Epuka matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu.
UZALISHAJI NA UPANDAJI WA VITUNGUU
 Kabla ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari.
EPUKA
 Kununua mbegu za mitaani, kuzidisha sana mbolea na umwagiliaji usio na mpangilio kwani husababisha vinguu kuzaa pacha. Pia epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani.
KITALU CHA VITUNGUU
Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini.

AINA ZA VITUNGUU VINAVYOLIMWA TANZANIA
 Red Creole, Bombay Red, Hybrid F1

 UTUNZAJI WA SHAMBA
Kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua inashauriwa ili kuongeza ruba ya ardhi, zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuiya utuamishaji wa maji na mlipuko wa magojwa ya miche. Kungoa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.
MAHITAJI YA MBOLEA
Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji ilioiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5 -12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1.
 UVUNAJI
Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye nyuzijoto chini ya 4.4 °C ama juu ya nyuzijoto 25°C ili visiharibike. UUZAJI 
Vitunguu ni zao lenye bei nzuri ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri. Kwa hivi sasa (sep. 15) hapa Morogoro vitunguu kilo moja ni Tshs. 1500/=. Kama vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo Ekari moja huzaa gunia 70- 90 sawa na kg 7000-9000. Kama akipata soko la uhakika mkulima anaweza kupata hadi 13.5 milioni kwa msimu mmoja.

STORI FUPI KUHUSU KILIMO KILIVYO NIPA MAFANIKIO

Leo napenda nizungumzie kuhusu kilimo, kazi ambayo kwa miaka mingi tangu shuleni tulifundishwa kuwa ndiyo UTI WA MGONGO WA UCHUMI WA NCHI YETU. Sina uhakika kauli hii bado ina ukweli ndani yake (maana ukweli wa jana unaweza kuwa uongo wa leo na kinyume chake). Ninachofahamu na ambacho bado ni ukweli ni kwamba; asilimia kubwa ya Watanzania wamategemea kilimo kuendesha maisha yao. Vijana wengi maofisini leo wamesomeshwa kwa kupitia kilimo. Huu ni ukweli.

Lakini kilimo hikihiki kilichotusaidia Watanzania wengi leo hii kinapuuzwa na asilimia kubwa ya watu, hasa vijana. Ni hapa Tanzania kuitwa mkulima ni tusi, siyo sifa! Nimekua nikisikia vijana wakitukana wenzao: "We mkulima nini?" Wapo watu wana ngeo leo walizozipata kwa sababu waliwatukana watu tusi hilo; MKULIMA.

Kwa unyanyapaaji huu wa kilimo, watu wengi, nikiwemo mimi, tulijikuta timekichukia kilimo na kukiona si biashara. Hata tulipotakiwa kufikiria mawazo ya biashara, kilimo hakikuwemo kwenye orodha, tulikiwazia vibaya! Hatukukipenda na tulipojaribu kukifanya tuliishia kutofanikiwa sababu hatukuwa na mapenzi nacho.

Mwaka 2002 nilizinduka katika usingizi mzito wa kutokiona kilimo ni biashara, nikasema “No”! Haiwezekani, kuna siri imejificha katika kilimo. Inawezekanaje! mi' mtoto wa mkulima nidharau kilimo? 


Swali hili lilinifanya niamue kutafuta shamba huko Itende na kuanzisha kilimo cha mananasi. Naweza kusema kwa sauti ya juu kwamba nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kulima mananasi huko Kiwangwa. Hakika nilipata mafanikio makubwa sana katika kilimo cha mananasi. Kwa waliowahi kufika Kiwangwa, watakuwa mashahidi wa jambo hili.
Hapo ndipo nilipothibitisha kwamba; kilimo si ushamba, si tusi, bali kuna siri kubwa sana imefichwa kwenye unyanyapaaji huu wa kilimo. Ndiyo maana leo napaza sauti yangu na kusema; KILIMO NI WAZO LA BIASHARA LINALOWEZA KUMWONDOA KIJANA WA KITANZANIA KWENYE UMASIKINI.

Hili hapa ni angalizo; KAMWE USIJARIBU KUFANYA BIASHARA YA KILIMO KAMA HUKIPENDI! Lazima kwanza uanzishe mapenzi na kilimo kabla ya kuanza biashara hii na uwe tayari kuvumilia. Katika biashara ya kilimo msamiati wa HARAKA, uweke pembeni.
Tafuta zao lolote unalotaka kulima, linaweza kuwa ufuta, mboga, matikiti, mahindi, n.k. Fanya utafiti wako ikiwa ni pamoja na kutafuta ardhi bora. 

Anza kidogokidogo, kisha panua kadri siku zinavyokwenda!
Jambo hili linawezekana, usikubali visingizio. Anza, halafu utaona milango mingine imefunguka! 


Ni kweli Biblia inasema usianze kujenga mnara kabla ya kufanya hesabu kama unaweza kuumaliza! Fungu hili limewafanya Wakristo wengi kubaki walipo wakisubiri kila kitu kitimie ndipo waanze; 
HABARI NJEMA NI KWAMBA ANZA NA ULICHONACHO NA UTAMALIZA NA KILA KITU. 

Asanteni,
Ni mimi ndugu yenu,
Michael.

kupata habari hii kamili tembelea link hii: https://www.facebook.com/michaegoba

0 comments:

Post a Comment

Alhamisi, 5 Novemba 2015

PATA HELA KUPITIA BLOG YAKO KWA KUTUMIA PROGRAM HII


Ndio unaweza kupata hela katika blogu yako kwa kutumia programu ya Google Adsense.
Google Adsense ni programu  ambayo inatumiwa na  wamiliki wa blogu na tovuti (Publishers), kuonyesha matangazo ya Google (Google Adwords)

Unachotakiwa kufanya ni kujisajili katika programu hii Google Adsense, wao wataikagua blogu yako na kama blogu yako au tovuti yako itakizi mahitaji yao basi watakupa kibali na namna ya kuweza wewe kuweka matangazo yao kwako.

Matangazo haya  ya Google Adsense yatakupa wewe hela kwa KUBOFWA (Clicks) naKUONEKANA (Impressions).

Angalizo
Hutakiwi Kubofya (Click) matangazo haya wewe mwenyewe. Acha watu wanaotembelea blogu au tovuti yako wabofye wao kwa mahitaji yao. Google Adsense wanayo namna ya kuangalia kama unafanya mchezo wa kubofya matangazo wewe mwenyewe na wakigundua hili hakuna onyo wanakufungia huduma hiyo.
Sasa ili uweze kupata Bofya (clicks) za kutosha pamoja na muonekano (Impressions) lazima blogu au Tovuti yako iwe na watembeleaji wa kutosha. Na namna ambavyo utapanga matangazo yako ili iwe na urahisi kwa watembeleaji kujionea matangazo kwa urahisi.

Kanuni ya iko hivi

WATEMBELEAJI WENGI + BOFYA ZA KUTOSHA = HELA ZA KUTOSHA 

Nisikuchoshe kwa leo hadi wakati mwingine tena. Kwa maoni au maswali niandikie kwa barua pepe mickyando12@gmail.com